Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

ISO 9001:2015 Imethibitishwa Kutoa Huduma za Hali ya Hewa kwenye Usafiri wa Anga

10 Days Forecast

MUHTASARI WA MWENENDO WA HALI YA HEWA KWA TAREHE 21-31 MEI, 2026 NA MATARAJIO YA HALI YA HEWA KWA TAREHE 01-10 JUNE, 2026.

MWELEKEO WA HALI YA HEWA KWA TAREHE 01-10 JUNE, 2026.

Kanda ya ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Mvua zinazoambatana na ngurumo za radi zinatarajiwa katika maeneo machache.

Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache.

Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache.

Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa.

Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Hali ya ukavu inatarajiwa.

Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa.

Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Vipindi vya mvua nyepesi vinatarajiwa katika maeneo machache.

Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa.

Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua