Seasional Forecast
MWELEKEO WA MSIMU WA KIPUPWE ( JUNI – AGOSTI), 2026
Dondoo muhimu za hali ya hewa kipindi cha Juni-Agosti (JJA), 2026
Taarifa hii inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa hali ya joto, upepo na mvua katika msimu wa Juni hadi Agosti (JJA), 2026; Ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbalimbali wanaotumia taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao. Kwa kawaida, kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti (JJA), hutawaliwa na hali ya baridi na upepo mkali kwa maeneo mengi ya nchi. Kwa muhtasari, mwelekeo wa msimu wa JJA, 2026 unaonesha kuwa:
Mwelekeo wa hali ya joto
- Hali ya baridi ya wastani hadi joto kiasi inatarajiwa katika maeneo ya Kanda ya Ziwa Victoria, Kanda ya magharibi, Kanda ya kusini, Nyanda za juu kusini-magharibi pamoja na Mkoa wa Singida. Hata hivyo, hali ya joto kiasi hadi baridi ya wastani inatarajiwa katika maeneo ya Ukanda wa pwani ya kaskazini na maeneo ya nchi kavu, Nyanda za juu kaskazini mashariki, Ukanda wa pwani ya kusini pamoja na mkoa wa Dodoma.
- Vipindi vya baridi zaidi vinatarajiwa kujitokeza katika mwezi Julai, 2026.
- Vipindi vya mvua za nje ya msimu vinatarajiwa katika maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria hususan Mkoa wa Mara, ukanda wa mwambao wa pwani na maeneo ya nchi kavu pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, na sehemu zenye miinuko za nyanda za juu kaskazini mashariki.
Mwelekeo wa hali ya upepo
- Msimu wa Kipupwe 2026 unatarajiwa kutawaliwa na upepo uliopupungua nguvu kidogo kama ilivyo kawaida utakaovuma kutoka Kusini Mashariki kwa maeneo mengi ya nchi, na vipindi vichache vya upepo mkali utakaovuma kutoka kusini hususan katika kipindi cha miezi ya Juni na Julai 2026 katika maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi na maeneo ya nchi kavu.
Athari
- Magonjwa yanayohusiana na hali ya hewa ya baridi kama vile homa ya mapafu na magonjwa ya mifugo yanaweza kujitokeza.
-
Hali ya vumbi linalosababishwa na upepo katika baadhi ya maeneo linaweza kupelekea uwepo wa magonjwa kama vile ya macho, mafua na magonjwa mengine yanayohusiana nayo.
Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua

