Taarifa za Utabiri
Upepo mkali na mawimbi makubwa kwa Ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi .................
Kwa taarifa zaidi, tafadhali pakua.
MWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 21-30 JUNI, 2022.
Kanda ya ziwa Viktoria (Mikoa ya Kagera, Geita,
Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Maeneo haya yanatarajiwa
kuwa na vipindi vifupi vya mvua na ngurumo za radi.
Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha,
Manyara na Kilimanjaro): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu na yenye hali ya
ubaridi.
Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Vipindi vifupi vya mvua nyepesi pamoja
na upepo wa wastani hadi mkali unatarajiwa.
Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na
Tabora): Maeneo
haya yanatarajiwa kuwa makavu kwa ujumla.
Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu
kwa ujumla yakiambatana na hali ya ubaridi.
Nyanda za juu
Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Maeneo
haya yanatarajiwa kuwa makavu kwa ujumla yakiamabatana na hali ya ubaridi.
Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu yakiambatana hali
ya ubaridi pamoja na vipindi vifupi vya mvua nyepesi..
Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu kwa
ujumla yakiambatana na hali ya ubaridi.
Imetolewa na; MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Kwa taarifa zaidi, tafadhali pakua...
Dondoo za tathmini ya Mei, 2022 na mwelekeo wa Juni, 2022:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Mei, 2022 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa hususan hali ya joto la chini kwa mwezi Juni, 2022 nchini.
- Katika kipindi cha mwezi Mei, mvua za Masika ambazo ni mahususi kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua ziliendelea kunyesha katika maeneo machache. Hata hivyo, vipindi vichache vya mvua kubwa vilijitokeza katika maeneo machache ya pwani ya kaskazini.
- Katika mwezi Juni, 2022 hali ya joto la chini inatarajiwa kupungua hususan nyakati za usiku na asubuhi katika maeneo mengi ya nchi ikiashiria kuanza kwa msimu wa Kipupwe. Vipindi vya upepo mkali pia vinatarajiwa hususan katika maeneo ya ukanda wa pwani. Aidha, vipindi vichache vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache ya ukanda wa pwani na Ziwa Victoria.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali pakua
Dondoo muhimu za hali ya hewa kipindi cha Juni-Agosti (JJA), 2022
Taarifa hii inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na hali ya hewa inayotarajiwa katika msimu wa Kipupwe katika kipindi cha Juni hadi Agosti (JJA), 2022; Ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbalimbali wanaotumia taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao. Kwa kawaida, kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti (JJA), huwa ni kipindi cha baridi na upepo kwa maeneo mengi ya nchi. Kwa muhtasari, mwelekeo huo kwa mwaka 2022 pamoja na athari zake unaonesha kuwa:
a)Viwango vya joto
- Katika kipindi cha JJA, 2022 hali ya baridi ya wastani hadi joto kiasi inatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi. Hata hivyo, hali ya joto kiasi hadi baridi ya wastani inatarajiwa katika maeneo ya ukanda wa pwani ya kaskazini pamoja na nyanda za juu kaskazini mashariki.
- Vipindi vya baridi zaidi vinatarajiwa kujitokeza mwezi Juni na Julai.
- Vipindi vya baridi kali vinatarajiwa katika maeneo ya miinuko ya nyanda za juu kusini magharibi hususan nyakati za usiku na asubuhi.
b)Upepo
Katika kipindi cha miezi ya Juni na Agosti, 2022 vipindi vya upepo mkali vinatarajiwa kushamiri katika maeneo mengi nchini. Msimu wa Juni hadi Agosti 2022 unatarajiwa kuwa na upepo utakaovuma kutoka kusini-mashariki na mashariki (Matlai) katika ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi na maeneo ya nchi kavu hususan mwezi Agosti, 2022.
c)Athari
- Magonjwa ya mifugo yanayoambatana na baridi kama vile homa ya mapafu yanaweza kujitokeza
- Hali ya vumbi inayoambatana na upepo mkali katika baadhi ya maeneo inatarajiwa kujitokeza na inaweza kuathiri afya ya binadamu na wanyama
Kwa maelezo zaidi, tafadhali pakua
Dar es Salaam |
|||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Tarehe | Hali ya Mchana | Kiwango cha Juu cha Joto | Kiwango cha Chini cha Joto | Mawio ya Jua | Machweo ya Jua | ||
28/06/2022 |
![]() Mvua Nyepesi |
30°C | 20°C | 06:34 | 18:14 | ||
29/06/2022 |
![]() Mvua Nyepesi |
29°C | 20°C | 06:34 | 18:14 | ||
30/06/2022 |
![]() Mvua Nyepesi |
29°C | 20°C | 06:34 | 18:14 | ||
01/07/2022 |
![]() Vipindi vya Jua |
30°C | 20°C | 06:36 | 18:18 | ||
02/07/2022 |
![]() Vipindi vya Jua |
30°C | 20°C | 06:36 | 18:18 |