Huduma Zetu

services images

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inatoa huduma za hali ya hewa katika usafiri wa anga ili kukidhi mahitaji na matarajio ya wateja kuendana na sheria na miongozo iliyopo kitaifa na kimataifa. Huduma zitolewazo na Mamlaka zimethibitishwa na Shirika la Viwango la Kimataifa ISO 9001:2015.

Huduma hizo ni kama ifuatavyo:

  1. Taarifa za hali ya hewa kwa ajili ya kutua na kuruka kwa ndege (METAR)
  2. Taarifa Maalum za hali ya hewa kwa ajili ya kutua na kuruka kwa ndege (SPECI) taarifa hizi hutolewa pindi kunapokuwa mabadiliko ya hali ya hewa ambayo hayakutolewa katika kipindi cha awali
  3. Utabiri wa hali ya hewa katika kiwanja cha ndege (TAF)
  4. Taarifa ya hali mbaya ya hewa katika anga za juu, kwa ajili ya ndege ikiwa angani (SIGMET).
  5. Taarifa za hali ya hewa kwa ajili ya ndege katika kiwanja inakotoka, inakoelekea na baadhi ya viwanja katika maeneo inakopita (flight documentation)
  6. Taarifa za uangazi wa hali ya hewa kutoka kwenye ndege angani (AIREP)
  7. Tahadhari na angalizo kwa ajili ya hali mbaya katika kiwanja (Aerodrome Warnings and Wind shear alerts)
  8. Taarifa za hali ya hewa kwa ajili ya uokozi wa ndege (Search and Rescue)
  9. Huduma za hali ya hewa kwa wateja wa usafiri wa anga kwa ajili kupata taarifa za wakati huo na maeneo mengine yanayotarajiwa kutumika na mteja.

Huduma hizi zinaweza kupatikana kupitia www.meteo.go.tz/ais