Machapisho
TAARIFA YA HALI MBAYA YA HEWA KWA MWEZI JANUARI NA FEBRUARI, 2024
PakuaKatika kipindi cha miezi ya Januari na Februari, 2024 vipindi vya mvua viliendelea kujitokeza katika maeneo mengi ya nchi. Aidha, maeneo mengi yalipata mvua za juu ya wastani hadi wastani ikilinganishwa na wastani wa muda mrefu wa miezi ya Januari na Februari. Vipindi vya mvua kubwa vilijitokeza katika baadhi ya maeneo. Hali hii ilisababisha mafuriko, ongezeko la unyevu ardhini na kina cha maji. Kwa upande mwingine, vipindi vya upepo mkali vilijitokeza katika maeneo machache ya ukanda wa Pwani na nyanda za juu kaskazini mashariki. Hali ya hewa iliyojitokeza pamoja na athari zake imeendana na taarifa ya mwelekeo wa mvua za Msimu, 2023/2024.