Machapisho
UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI MACHI, 2024
PakuaDondoo za tathmini ya Februari, 2024 na mwelekeo wa Machi, 2024:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Februari, 2024 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Machi, 2024 nchini.
i.Katika kipindi cha mwezi Februari, 2024 maeneo mengi yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka yaliendelea kupata mvua za juu ya wastani pamoja na vipindi vya mvua kubwa katika baadhi ya maeneo na kusababisha athari ikiwemo mafuriko na uharibifu wa mali na miundombinu.
ii.Katika kipindi cha mwezi Machi 2024, mvua za msimu zinatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka. Hata hivyo, mvua za Masika zilizoanza mwishoni mwa mwezi Februari, 2024 zinatarajiwa kuendelea katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Ongezeko la mvua linatarajiwa katika baadhi ya maeneo nchini.
iii.Joto la kawaida hadi juu kidogo ya kawaida linatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi kwa kipindi cha mwezi Machi, 2024.