Machapisho

MWELEKEO WA MVUA ZA MASIKA (MACHI – MEI), 2024 KWA MKOA WA ARUSHA

Pakua

(i) Hali ya El Niño inayoendelea kwa sasa katika Bahari ya Pasifiki inatarajiwa kupungua nguvu hasa tunapoelekea katika msimu wa mvua za Masika, 2024.
(ii) Kwa ujumla mvua za Wastani hadi Juu ya Wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya mkoa wa Arusha.
(iii) Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Februari, 2024.
(iv) Mvua zinatarajiwa kuisha kati ya wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Mei, 2024.
(v) Upo uwezekano wa kutokea vipindi vya ukavu vya siku kumi (10) au zaidi katika msimu huu wa Masika, 2024.