Dira na Dhamira


Dira ya Mamlaka ya Hali ya Hewa:

Kuwa kitovu bora cha utoaji huduma za hali ya hewa zenye hadhi ya kimataifa.

Dhima ya Mamlaka ya Hali ya Hewa:

Kutoa huduma za hali ya hewa zilizo bora, zinazokidhi matarajio ya wadau na hivyo kuchangia katika kulinda maisha ya watu na mali zao, mazingira na pia kuchangia katika azma ya Taifa ya kupunguza umasikini.

Maadili Muhimu:

Katika kutekeleza dhima na dira Mamlaka itahakikisha yafuatayo yanafanyika:

  1. Utendaji unaozingatia taaluma
  2. Utendaji kazi wa pamoja
  3. Utawala Bora
  4. Utoaji huduma bora
  5. Kutoa huduma kwa muda unaotakiwa
  6. Kumjali Mteja