Historia

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ni Taasisi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria namba 2 ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutiwa saini tarehe 13 Februari 2019 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt John Pombe Joseph Magufuli.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ilizinduliwa rasmi na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mheshimiwa Mhandisi Isack Kamwelwe tarehe 05 septemba 2019.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ni Taasisi Mahususi na pekee katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye Mamlaka ya kutoa huduma za Hali ya Hewa ndani ya Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Makao Makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania yapo Jijini Dar es salaam, aidha Mamlaka inatoa huduma zake pia kupitia vituo vyake vilivyopo katika maeneo mbalimnali mikoani.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inafanyakazi chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.