Taarifa za Hali ya Hewa Kilimo
Jarida la Hali ya Hewa kilimo la Tathimini ya 11- 20 Machi 2024 na Utabiri wa Machi 21- 31, 2024
PakuaDONDOO ZA MACHI 21 - 31, 2024
- Katika kipindi cha Machi 21-31 2024, hali ya mvua inatarajiwa katika maeneo mengi nchini ambayo itasaidia ukuaji na maendeleo ya mazao
- Wakulima katika maeneo yanayopata mvua za Masika wanashauriwa kuendelea kupanda mazao huku wakipata ushauri kutoka kwa maafisa kilimo katika maeneo yao
- Wakulima na wafugaji wanashauriwa kuendelea kufuatilia kwa ukaribu hali ya mazao, mashamba, mifugo na malisho ili kuweza kukabiliana na athari mbalimbali zinazoweza kujitokeza.
Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua....
Jarida la Hali ya Hewa Kilimo la msimu wa mvua wa Machi hadi Mei 2023
PakuaMUHTASARI
- Mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka isipokuwa maeneo machache ya mikoa ya Dar es salaam, Pwani (ikijumuisha Mafia), kaskazini mwa Morogoro pamoja na kisiwa cha Unguja ambapo mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa.
- Ongezeko la mvua linatarajiwa katika kipindi cha mwezi Mei 2023, hususan katika maeneo ya pwani ya kaskazini.
- Mvua za Masika zinatarajiwa kuanza mwezi Machi, katika maeneo mengi na zinatarajiwa kuisha katika wiki ya nne ya mwezi Mei 2023 katika maeneo mengi ingawa mwendelezo wa mvua za nje ya msimu unatarajiwa mwezi Juni 2023 katika maeneo machache ya ukanda wa pwani ya kaskazini.
- Mvua chache na zenye mtawanyiko usioridhisha katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani zinaweza kusababisha upungufu wa unyevu kwenye udongo na upatikanaji wa maji kwa ajili ya shughuli za kilimo.
- Katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani, unyevu wa udongo kupita kiasi unaweza kujitokeza na hivyo kuathiri ukuaji wa mazao ambayo hayahitaji maji mengi.
Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua...