Taarifa za Hali ya Hewa Kilimo
Jarida la Hali ya Hewa kilimo la Tathimini ya 11 - 20 Juni 2022 na Utabiri wa Juni 21 - 30, 2022
PakuaDONDOO ZA JUNI 21 - 30, 2022
- Hali ya ukavu inayotarajiwa itasaidia shughuli za uvunaji, ukaushaji na uhifadhi wa mazao.
- Wafugaji wanashauriwa kutumia maji na malisho kwa uangalifu.
- Wakulima wanashauriwa kupanda mazao ya mboga mboga na mizizi katika maeneo yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji.
- Kutoka na hali ya upepo inayotarajiwa hususani kwa maeneo ya mikoa ya kanda ya Pwani, wavuvi wanashauriwa kufuatiliataarifa za hali ya hewa za kila siku ili kufanya maamuzi juu ya wakati sahihi wa kwenda kufanya shughuli za uvuvi.
- Hali ya baridi inayotarajiwa inaweza kuwa na athari kwa mazao na wanyama.
Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua
Jarida la Hali ya Hewa Kilimo la msimu wa mvua wa November 2021 hadi Aprili 2022
PakuaMUHTASARI
- Utabiri wa mvua za mwezi Novemba hadi Aprili (NDJFMA) ni mahususi kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka.
- Mvua zinatarajiwa kuwa za chini ya wastani hadi wastani katika maeneo mengi ya mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Singida, Dodoma, Rukwa, Songwe, Mbeya na Iringa na wastani hadi chini ya wastani katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Njombe, Ruvuma, Lindi, Mtwara na kusini mwa mkoa wa Morogoro.
- Vipindi virefu vya ukavu vinatarajiwa kati ya mwezi Novemba, 2021 na Januari, 2022.
- Mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya tatu ya mwezi Novemba, 2021 katika maeneo mengi na kuisha katiya wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Aprili, 2022.
- Malisho na maji ya mifugo vinatarajiwa kupungua hivyo kupelekea kongezeka kwa migororo ya wakulima nawafugaji.
Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua...