Taarifa za Utabiri
ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo
machache ya mikoa ya Mara, Simiyu, Mwanza,
Shinyanga, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida,
Dodoma, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Tabora,
Tanga, Dar es Salaam, Morogoro, Pwani (ikijumuisha
visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa
vya Unguja na Pemba.
MWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 21-31 MACHI, 2025
Kanda ya ziwa Viktoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara):
Vipindi vya mvua kubwa zinazoambatana na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache.
Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache.
Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaampamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Vipindi vya mvua zinazoambatana na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache.
Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Vipindi vya mvua kubwa zinazoambatana na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache.
Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache.
Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Vipindi vya mvua kubwa zinazoambatana na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache.
Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Vipindi vya mvua zinazoambatana na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache.
Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Vipindi vya mvua kubwa zinazoambatana na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache.
Imetolewa na;
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Kwa maelezo zaidi tafadhali pakua...
Dondoo za tathmini ya Februari, 2025 na mwelekeo wa Machi, 2025:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Februari, 2025 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Machi, 2025 nchini.
- Katika kipindi cha mwezi Februari, 2025 vipindi vya ukavu pamoja na hali ya joto vilijitokeza katika maeneo mengi ya nchi hususan kuanzia wiki ya pili ya mwezi. Aidha, baadhi ya maeneo yalipata mvua pamoja ngurumo. Aidha, vipindi vya mvua kubwa vilijitokeza katika maeneo machache na kusababisha athari ikiwemo mafuriko na kutuama kwa maji.
- Katika kipindi cha mwezi Machi 2025, mvua za Masika zinatarajiwa kuanza katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka, na mvua za Msimu zinatarajiwa kuendelea katika maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka. Aidha, ongezeko la mvua linatarajiwa katika maeneo machache.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali pakua
Dondoo muhimu za mvua za Masika (Machi – May), 2025
Taarifa hii inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa mvua za Masika kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka (kanda ya Ziwa Victoria, nyanda za juu kaskazini mashariki, pwani ya kaskazini pamoja na maeneo yaliyopo kaskazini mwa mkoa wa Kigoma) katika kipindi cha miezi ya Machi hadi Mei, 2025. Ushauri na tahadhari umetolewa kwa wadau wa sekta mbalimbali wanaotumia taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao kama vile kilimo na usalama wa chakula, mifugo na uvuvi, maliasili, wanyamapori na utalii, nishati na maji, usafirishaji (nchi kavu, kwenye maji na angani), mamlaka za miji, afya, sekta binafsi pamoja na menejimenti za maafa. Muhtasari wa mwelekeo wa mvua hizo na athari zake ni kama ifuatavyo:
a) Mwelekeo wa mvua za Masika kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka:
i. Mvua za Wastani hadi Chini ya Wastani zinatarajiwa katika maeneo ya pwani ya kaskazini, kaskazini mwa mkoa wa Kigoma na ukanda wa Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga na magharibi mwa mikoa ya Simiyu na Mara). Aidha, Mvua za Wastani hadi Juu ya Wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nyanda za juu kaskazini mashariki pamoja na mashariki mwa mikoa ya Mara na Simiyu.
ii. Mvua za Masika zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Machi , 2025 katika maeneo ya kanda ya Ziwa Victoria na pwani ya kaskazini; na katika wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Machi, 2025 katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki.
iii. Ongezeko la mvua linatarajiwa mwezi Aprili, 2025
b) Athari zinazotarajiwa:
i. Vipindi vya unyevu wa kuzidi kiasi pamoja na mafuriko vinaweza kujitokeza na kuathiri ukuaji wa mazao hususan katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za Wastani hadi Juu ya Wastani.
ii. Kina cha maji katika mito na mabwawa kinatarajiwa kuongezeka hivyo kuongeza hatari ya mafuriko hususan katika maeneo yanayoathiriwa na mafuriko.
iii. Magonjwa ya mlipuko yanaweza kujitokeza kutokana na uchafuzi wa maji.
Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua
Dar es Salaam |
|||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Tarehe | Hali ya Mchana | Kiwango cha Juu cha Joto | Kiwango cha Chini cha Joto | Mawio ya Jua | Machweo ya Jua | ||
29/03/2025 |
![]() Mvua na Ngurumo |
30°C | 25°C | 06:28 | 18:33 | ||
29/03/2025 |
![]() Mvua na Ngurumo |
34°C | 25°C | 06:28 | 18:33 | ||
30/03/2025 |
![]() Mvua na Ngurumo |
34°C | 25°C | 06:28 | 18:33 | ||
29/03/2025 |
![]() Mvua na Ngurumo |
34°C | 25°C | 06:28 | 18:33 | ||
30/03/2025 |
![]() Mvua na Ngurumo |
34°C | 25°C | 06:28 | 18:33 |