Machapisho

Mwelekeo wa mvua kwa mwezi Novemba 2019

Pakua

MUHTASARI WA HALI YA HEWA KWA MWEZI OKTOBA, 2019 NA MWELEKEO KWA MWEZI NOVEMBA, 2019

Dondoo za Novemba, 2019

Taarifa hii inatoa muhtasari wa hali ya viashiria pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Oktoba, 2019 na mwelekeo wa viashiria pamoja na mwenendo wa mvua kwa mwezi Novemba, 2019 nchini.

a)Maeneo mengi ya nchi yanayopata misimu miwili ya mvua (Nyanda za juu kaskazini mashariki, Pwani ya kaskazini pamoja na Ukanda wa Ziwa Viktoria) yamepata mvua katika mwezi Oktoba, 2019. Aidha, vipindi kadhaa vya mvua kubwa vimeripotiwa hususan katika maeneo ya pwani ya kaskazini pamoja na Ukanda wa Ziwa Viktoria.

b)Mvua za Msimu (NDJFMA 2019-2020) katika maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka (kanda ya magharibi, kati, nyanda za juu kusini magharibi, kusini mwa nchi, ukanda wa pwani ya kusini pamoja na maeneo ya kusini ya mkoa wa Morogoro) zinatarajiwa kuanza katika mwezi Novemba, 2019.

c)Upungufu wa mvua unatarajiwa katika maeneo mengi ya Pwani ya kaskazini na nyanda za juu kaskazini mashariki hususan katika wiki ya kwanza ya mwezi Novemba, 2019. Hali hii inasababishwa na uwepo wa kimbunga ‘Kyarr’ na migandamizo midogo ya hewa iliyopo kaskazini magharibi mwa bahari ya Hindi (NWIO), ambapo upepo wenye unyevunyevu kutoka baharini unatarajiwa kuvutwa kuelekea katika kimbunga hicho.

Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua