Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

ISO 9001:2008 Certified in Aviation Meteorological Services

Utabiri wa siku 10

MUHTASARI WA MWENENDO WA MVUA KWA SIKU KUMI (01– 10 JANUARI, 2017) NA MATARAJIO YA MVUA KWA SIKU KUMI (11– 20 JANUARI, 2017)

1.1 MUHTASARI WA MWENENDO WA VIASHIRIA NA MFUMO WA MVUA KWA SIKU KUMI (01– 10 JANUARI, 2017)

Katika siku kumi za kwanza za Januari 2017, migandamizo mikubwa ya hewa iliyo sehemu za Kusini mwa Dunia (S. Helena na Mascarene) iliendelea kupungua nguvu wakati ile ya sehemu za Kaskazini (Azores na Siberia) iliendelea kuimarika na hivyo kuruhusu ukanda wa mvua wa ITCZ kukaa sehemu ya kusini ya nchi yetu (Tanzania). Hali ya joto la bahari la wastani katika Bahari ya Atlantiki karibu na pwani ya Angola ilirekodiwa. Joto la wastani hadi juu ya wastani lilirekodiwa Kusini-magharibi mwa Bahari ya Hindi. Kutokana na kudhoofika kwa migandamizo mikubwa ya hewa katika maeneo ya Kusini mwa Dunia, pepo hafifu kutoka Kusini-mashariki na mashariki zilileta mvua chache katika ukanda wa pwani. Hali hii pia ilisababisha mvua na ngurumo katika maeneo ya Magharibi mwa nchi.

1.2 MUHTASARI WA MWENENDO WA MVUA KWA SIKU KUMI (01– 10 JANUARI, 2017)

Katika kipindi hiki mvua na ngurumo vilirekodiwa katika Ukanda wa Ziwa Viktoria na y ale ya Magharibi na kusini mwa nchi. Kwa upande mwingine, ukanda wa pwani ya kaskazini na nyanda za Juu Kaskazini-mashariki yalikuwa makavu kwa ujumla.

MATARAJIO YA HALI YA HEWA KATIKA SIKU KUMI (11– 20 JANUARI, 2017)

1.2.1 VIASHIRIA NA MFUMO WA MVUA KWA SIKU KUMI (11– 20 JANUARI, 2017)

Katika siku kumi za pili za Januari 2017, migandamizo mikubwa ya hewa iliyo sehemu za Kusini mwa Dunia (S. Helena na Mascarene) inatarajiwa kupungua nguvu wakati ile ya sehemu za Kaskazini (Azores na Siberia) inatarajiwa kuimarika na hivyo kuruhusu ukanda wa mvua wa ITCZ kukaa katika maeneo ya kusini mwa nchi; hata hivyo, ukanda huu unatarajiwa kuwa dhaifu. Hali ya joto la bahari la wastani hadi chini ya wastani katika Bahari ya Atlantiki karibu na pwani ya Angola inatarajiwa kuendelea. Hali hii inatarajiwa kupelekea mvua kubakia zaidi katika maeneo ya Magharibi, kusini magharibi na kusini mwa nchi. Joto la wastani hadi juu ya wastani linatarajiwa Kusini-magharibi mwa Bahari ya Hindi.

1.2.2 MWELEKEO WA MVUA KWA SIKU KUMI (11– 20 JANUARI, 2017)

Kanda ya ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Mara na Simiyu): Makavu kwa ujumla na vipindi vichache vya mvua zitakazoambatana na ngurumo katika maeneo machache vinatarajiwa.

Nyanda za juu kaskazini mashariki (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara): Makavu kwa ujumla na vipindi vichache vya mvua zitakazoambatana na ngurumo katika maeneo machache vinatarajiwa.

Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Makavu kwa ujumla na vipindi vichache vya mvua zitakazoambatana na ngurumo katika maeneo machache vinatarajiwa, hususan nusu ya pili ya kipindi.

Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Vipindi vya mvua zitakazoambatana na ngurumo katika maeneo machache vinatarajiwa, .

Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Vipindi vya mvua zitakazoambatana na ngurumo katika maeneo machache vinatarajiwa,

Nyanda za juu kusini magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Njombe, Iringa na Mbeya): Vipindi vya mvua zitakazoambatana na ngurumo katika maeneo machache vinatarajiwa, hususan nusu ya pili ya kipindi.

Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Vipindi vichache vya mvua zikiambatana na ngurumo zinatarajiwa, hususan nusu ya pili ya kipindi.

Kanda ya kusini (Mikoa ya Njombe na Ruvuma): Vipindi vya mvua zitakazoambatana na ngurumo katika maeneo machache vinatarajiwa.

Imetolewa na; MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA


Weather by Region

© 2017 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa.