Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

ISO 9001:2015 Certified in Aviation Meteorological Services

Habari

 • SADC MANYANYA

  Imewekwa: 08th August, 2019

  • Tarehe 8/08/2019; Naibu waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Mhandisi Stella M. Manyanya (MB) ameipongeza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kazi nzuri inayoifanya kwa kutoa taarifa sahihi za hali ya hewa kwa wananchi.

  Alizungumza hayo wakati alipotembelea banda la TMA katika Maonesho ya Wiki ya Viwanda ya SADC, viwanja vya ukumbi wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

  ‘Nawapongeza sana TMA kwa kazi nzuri mnayoifanya kwa sasa ya umakini ambao umehakikisha kiwango cha usahihi kimekuwa juu hivyo kutoa tabiri za kweli’

  Aliongezea kwa kusema kutokana na usahihi huo, wizara ya viwanda imeweza kunufaika katika maendeleo ya ukuaji wa viwanda hususani upatikanaji wa malighafi za kilimo n.k

  Kwa upande mwingine alitoa pongezi zake za dhati kwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi kwa kuchaguliwa kuwa Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani na hivyo kuiletea sifa nchi na kuwakilisha vyema wanawake wa Tanzania kimataifa

  Alimalizia kwa kuwataka wafanyakazi wa TMA kuendelea kuchapa kazi kwa vile mchango wao unaonekana katika maendeleoya nchi

  kwa matukio zaii ingia humu http://meteotz1950.blogspot.com/2019/08/naibu-waziri-wa-viwanda-na-biashara.html

 • Weather by Region

  © 2019 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa.