Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

ISO 9001:2015 Certified in Aviation Meteorological Services

Habari

 • UZINDUZI TERMINAL III:

  Imewekwa: 06th August, 2019

  Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Buruhani Nyenzi amefurahishwa na jitihada za wafanyakazi wa TMA JNIA za kuhakikisha ofisi ya TMA katika jengo la tatu la abiria JNIA zimeanza kutoa huduma za hali ya hewa kwa wasafiri wa anga kwa wakati muafaka.

  Alizungumza hayo wakati alipotembelea ofisi hizo mara baada ya ufunguzi rasmi wa jengo hilo,

  ‘Nimefurahishwa na jitihada za wafanyakazi za kuhakikisha ofisi hii inaanza kazi kwa wakati mara tu baada ya uzinduzi rasmi na itafanya kazi masaa 24’,alizungumza Dkt. Nyenzi

  Aliongezea ‘nasisitiza utunzaji wa samani na vitendea kazi vya ofisi ili kuendelea kuweka taswira nzuri kwa wapokea huduma yaani wateja’,

  Naye, Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi aliyeambatana na mwenyekiti huyo alionesha furaha yake kwa kujivunia namna ambavyo wafanyakazi wa Mamlaka wanavyojituma kwa bidii na moyo wa uzalendo katika kutimiza majukumu yao ya kuwafikishia huduma wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na sekta ya usafiri wa anga.

  Awali wakati akitoa maelezo kuhusu ofisi hiyo, meneja wa huduma za hali ya hewa kwa usafiri wa anga TMA-JNIA Bw. John Mayunga alimweleza mwenyekiti kuwa ofisi hiyo itafanya kazi masaa 24 na imeandaa sehemu maalum kwa ajili ya kusikiliza na kutatua changamoto za wateja (cutomer help desk) zitakazojitokeza kama vile matumizi ya mfumo wa utoaji taarifa za hali ya hewa kwa usafiri wa anga (Meteorological Aviation Information System-MAIS)

  Jengo la tatu la abiria JNIA limezinduliwa rasmi tarehe 01 Agosti 2019 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa.

 • Weather by Region

  © 2019 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa.