Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

ISO 9001:2015 Certified in Aviation Meteorological Services

Habari

 • Mvua za msimu wa Novemba 2018 hadi Aprili 2019

  Imewekwa: 11th October, 2018

  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) leo tarehe 11/10/2018 imekutana na wadau kutoka sekta ya maafa, afya, kilimo, nishati, mazingira,mipango miji na wanahabari kujadili matarajio na mwelekeo wa mvua za msimu kwa maeneo yanayopata mvua mara moja kwa mwaka kuanzia mwezi Novemba 2018 hadi Aprili 2019 ili kuongeza uelewa wa taarifa za hali ya hewa kwa sekta mbalimbali zinazoathirika zaidi na hali ya hewa.


  Aidha, wadau walipata nafasi ya kujadili mwenendo wa utabiri wa msimu wa vuli (Oktoba hadi Desemba 2018) uliotolewa 05 Septemba 2018 ambao unaonesha kuwa mvua zimeanza (onset) kama ilivyotabiriwa kwa maeneo mengi ingawaje mtawanyiko wake bado haujaimarika hali inayosababishwa na mgandamizo mdogo wa hewa uliopo Mashariki mwa Pwani ya Somalia unaoathiri mifumo ya hali ya hewa


  Kwa upande wa mdau kutoka wizara ya afya bw.Stephen Kiberiti aliwashukuru TMA kwa utaratibu wa kukutana na wadau hii inasaidia sekta husika kujiandaa na athari zinazoweza kujitokeza.


  Mikoa inayopata mvua mara moja kwa mwaka ni Dodoma, Singida, Katavi, Mbeya,Tabora, Kigoma(ukitoa Kigoma Kaskazini), Mtwara, Lindi,Ruvuma, Iringa, Songwe, Rukwa, Njombe na Kusini mwa Morogoro


  Warsha hii imedhaminiwa na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kupitia mradi wa mfumo wa kidunia wa huduma za hali ya hewa Duniani (Global Framework for Climate Service-GFCS)


  IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO

  MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA (TMA)

 • Weather by Region

  © 2019 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa.