Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

ISO 9001:2015 Certified in Aviation Meteorological Services

Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu

 • Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu
  Dkt. Agnes Lawrence Kijazi

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania anawataka na kuwashauri wadau na umma wa Tanzania kwa ujumla kuwa wasikivu na wenye kuchukua hatua stahiki kufuatia madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa ambapo Tanzania ni moja ya nchi athirika duniani

  Wastani wa joto la dunia umeongezeka na hivyo mifumo ya hali ya hewa imebadilika na kusababisha joto kali, ukame na mafuriko kuwa hali ya kawaida katika maeneo yetu.Hii inamaanisha hali joto katika mikoa ya Tanzania kuongezeka na kusababisha madhara kwa afya za binaadamu na viumbe wengine,maeneo mengi yameendelea kuwa na ukame na kusababisha uhaba wa chakula na maji, mafuriko pia yamekuwa matokea ya kawaida na kuongezeka hivyo kuhatarisha maisha ya watu, wanyama na mali mbalimbali

  Mkurugenzi Mkuu anasisitiza jamii kuchukua hatua stahiki ikiwemo kupanda miti kama inavyosahuriwa na wataalamu ili kupunguza madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa na Tabia nchi kama njia mbadala ya kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa

  Kwa upande Mwingine, Mkurugenzi Mkuu anawataka wadau na jamii kwa ujumla kufuatilia Taarifa mbalimbali za hali ya hewa kama zinavyotolewa na Mamlaka ili kufanikisha shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi na hivyo kuwezesha upatikanaji wa matokea makubwa katika mipango binafsi na nchi kwa ujumla


 • Weather by Region

  © 2019 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa.