Matukio
Taarifa za Hali ya Hewa Kilimo
Jarida la Hali ya Hewa kilimo la Tathimini ya 01 - 10 April 2021 na Utabiri wa Aprili 11 - 20, 2021
PakuaDONDOO ZA APRILI 11- 20 2021
- Upungufu wa unyevunyevu wa udongo maeneo ya kanda ya kati hususan katika mkoa wa Dodoma umeathiri ukuaji wa mazao ya mahindi katika baadhi ya maeneo katika mkoa huo
- Mvua zinazotarajiwa katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua zinaweza kuathiri mashamba kwenye maeneo yanayotuamisha maji na yale yanayokumbwa na mafuriko mara kwa mara
Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua ...
Taarifa ya Msimu wa MAM (MASIKA) 2021 ya Hali ya Hewa Kilimo
PakuaMUHTASARI
- Utabiri wa mvua za masika (Machi-Mei) 2021, ni mahususi kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.
- Mvua za Masika zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi ya mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara pamoja na maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Kigoma (wilaya za Kakonko na Kibondo)
- Mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa katika maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, mikoa ya Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
- Mvua za Masika zinatarajiwa kuanza mapema katika wiki ya nne ya mwezi Februari, 2021 hususan katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki na pwani ya kaskazini.
- Magonjwa ya mlipuko yanaweza kujitokeza kutokana na kutuama kwa maji machafu na uchafuzi wa maji safi.
- Vipindi vifupi vya mvua kubwa vinaweza kuambatana na mafuriko, maporomoko ya udongo na kusababisha uharibifu wa miundombinu, shughuli za kijamii kuathirika, upotevu wa maisha na mali.
Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua...